Ebook: Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar
Author: Amrit Wilson, Ahmada Shafi Adam
- Year: 2016
- Publisher: Daraja Press
- City: Montreal
- Language: Kiswahili (Swahili)
- pdf
Kitabu hiki kinaturudisha katika kipindi cha kusisimuwa cha miaka ya vita baridi, kipindi ambacho, sambamba na kipindi cha leo, madola ya kibeberu yamekuwa yakifanya njama za kubadilisha serikali zilizokuwepo na kuziweka madarakani zile zenye kufuata amri. Kwa kutumia kumbukumbu za picha za Johari, nyaraka za siri za Marekani na Uingereza, pamoja na mahojiano ya kina, kitabu kinatowa uchambuzi juu ya nafasi na satwa ya Chama cha Umma Party nchini Zanzibar na kiongozi wake mwenye upeo mkubwa wa mambo, Mwanamapinduzi mfuasi wa Itikadi ya Karl Marx, Abdulrahman Mohamed Babu. Kwa kuangalia kwa njia ya uwiano wa mifano inayokwenda sambamba ya wahka wa Marekani kuhusu Uchina ya Kikomunisti katika miaka ya 1960 na woga walionao hivi sasa kuhusu ushawishi wa Uchina, kitabu kinatafakari juu ya mivutano mipya iliyopo katika kupigania rasilmali za Afrika, kuundwa kwa kikosi cha AFRICOM, na jinsi Wanasiasa wa Afrika Mashariki wanavyoshiriki katika kuimarisha udhibiti wa Marekani katika nchi zao, na "Vita dhidi ya Ugaidi" katika ukanda wa Afrika Mashariki hivi sasa.
Download the book Tishio la Ukombozi: Ubeberu na Mapinduzi Zanzibar for free or read online
Continue reading on any device:
Last viewed books
Related books
{related-news}
Comments (0)