Online Library TheLib.net » Historia ya Mapambano ya Mwafrika
cover of the book Historia ya Mapambano ya Mwafrika

Ebook: Historia ya Mapambano ya Mwafrika

00
13.02.2024
0
0
Kwa karne kadhaa wakoloni na wabaguzi wa rangi wamekuwa wakieneza fikara mbaya kwamba “Waafrika hawakuwa na historia” mpaka watu kutoka nchi za mbali walipoingia na kufanya biashara nasi au kututawala. Kwa wakoloni maana ya “histona” ni matukio ya kale na ya sasa ya Ulaya au yanayowahusu Wazungu, binafsi au kitaifa.

Wasomi wengi Waainmka kwanza waliikubali tafsari hii ya “historia”, wakaisoma, wakaitetea na kuieneza. Historia ya Tanzania, kwa mfano, kwao ingekuwa kwanza historia ya Waarabu kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki mpaka kuingia kwa utawala wa Wajerumani na Waingereza. Mengineyo juu ya Tanzania yasingeitwa historia wacha kusomeshwa.

Historia ya Mapambano ya Mwafrika kinachambua vizuri sana tatizo hili la “utovu wa historia ya Mwafrika” na hata kutupilia mbali maneno yaliyotumiwa kama vile “manegro, bushmen n.k.” ambayo yamejaa kasumba ya kashfa dhidi ya Waafrika. Lakini zaidi ya hayo kitabu hiki kina uchambuzi madhubuti wa kudhoofishwa kwa maendeleo ya kijamii — kiuchumi ya Waafrika na wageni na jinsi gani Waafrika wanaweza kujikomboa kikamilifu.

Katika safu ya vitabu vya historia, Historia ya Mapambano ya Mwafrika ni kitabu cha lazima.
Download the book Historia ya Mapambano ya Mwafrika for free or read online
Read Download
Continue reading on any device:
QR code
Last viewed books
Related books
Comments (0)
reload, if the code cannot be seen